fB insta twitter

Ujenzi kiwanja cha Ndege kwa Rais Magufuli wazua mjadala

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya story ambayo imeandikwa June 12 2016 kwenye gazeti la MTANZANIA ni hii yenye kichwa cha habari ‘Ujenzi kiwanja cha ndege Chato wazua nongwa’ Gazeti hilo limeripoti kuwa kusudio la Serikali kujenga kiwanja cha ndege wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita ambako ni nyumbani kwa Rais Dk. John Magufuli limezua mjadala mkubwa.

Gazeti hilo limesema kuwa juzi wakati mbunge wa CHADEMA David Silinde akisoma maoni ya kambi ya Upinzani bungeni, kuhusu hali ya uchumi wa Taifa, Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Makadirio ya Mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na mambo mengine alihoji juu ya ujenzi huo.

Mtanzania limeripoti kuwa wakati akisoma maoni hayo Silinde alidai tayari uwanja huo umekwishatengewa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya upembuzi yakinifu. Kambi hiyo ilihoji kama kuna utafiti wowote ambao Serikali imeufanya na unaonyesha kwamba ujenzi huo unamaslahi na ni kipaumbele cha Taifa kwa sasa.

Aidha Gazeti hilo limesema kuwa kambi hiyo ilishauri Serikali kwanini fedha hizo zilizokwishatengwa zisipelekwe kuimarisha viwanja vilivyopo sasa hasa ikizingatiwa kuwa serikali inataka kununua ndege tatu za shirika  Ndege la ATCL.

Kauli hiyo ya Upinzani ndiyo ambayo imezua mijadala hiyo katika mitandao mbalimbali ya kijamii huku baadhi wakimnyooshea kidole moja kwa moja Rais Magufuli juu ya hatua hiyo.

Waweza kuzipitia hapa nyingine kubwa kwenye magazeti ya leo June 12 2016

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV JUNE 12 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments