Mix

Mshindi mwingine wa ‘Airtel Yatosha Zaidi’ naye kakabidhiwa gari yake IST

on

pic 8

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Wilman Kapenjama akikabidhi funguo ya gari kwa Mshindi wa Promosheni Airtel yatosha Zaidi, Sefu Namtapika

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel imekabidhi zawadi ya gari Toyota IST kwa mshindi wa tatu wa droo ya kwanza Promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi inayofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo jumla ya magari 60 yatatolewa kwa wateja wanaotumia mtandao huo.

Gari hilo la tatu limetolea kwa mshindi kutoka Mtwara ambaye ni mwalimu mstaafu, Seif Namtapika katika hafla iliyofanyika Viwanja vya mashujaa.

pic 4

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Wilman Kapenjama akimpongeza mzee Sefu Namtapika baada ya kumkabidhi gari yake

Ndugu zangu sikuamini kabisa nilipopigiwa kuambiwa nimeshinda, wala nilikuwa sijui kama kuna siku ntamiliki gari na tena ukizingatia mimi nimeshastaafu, kweli nawashukuru Airtel pamoja na mungu wangu kwa kunipa zawadi hii”– Namtapika.

pic 6

.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Willman Ndile Kapenjama alihudhuria hafla ya makabidhiano ya gari hiyo.

hii ni njia bora kwa kampuni ya Airtel kurudisha faida kwa wananchii ambao kwa kiasi kikubwa wanatumia mtandao huo na ninawasihi endeeni kushirikiana na jamii kwa kila njia ili kubadilisha maisha na ndoto za wateja wengi”– Kapenjama.

Mkuu wa Mauzo wa kanda ya kusini, Albert Majuva anasema imekuwa faraja kwa mshindi kutoka katika kanda hiyo ambako watu wengi kutumia mtandao wa Airtel.

Promosheni hiyo ya Airtel yatosha zaidi bado itadumu kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo mtumiaji wa Airtel anaweza kujipatia muda wa maongezi zaidi, SMS zaidi na internet zaidi kwa ajili ya kuperuzi, kubwa zaidi ni nafasi kwa mteja mmoja kujishindia TOYOTA IST moja kila siku kwa muda wa miezi miwili.

pic 9

pic 10

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando

pic 11

Mzee Sefu Namtapika akipongezwa na mke wake.

Unataka niwe nakusogezea kila kinachonifikia? Ungana na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram kwa kubonyeza hapa ili niwe nakutumia kila kitu moja kwa moja >>>Facebook Twitter Instagram

Tupia Comments