Top Stories

Aishtaki kampuni iliyomuajiri kisa rasta zake

on

Mmarekani mweusi Jeffrey Thornton ameishtaki Kampuni iliyomuajiri ya Encore Group, kwa kumfanyia unyanyasaji baada ya kumwambia akate rasta zake ili aendane na mazingira ya kazini “niliambiwa nikate nywele zisiguse masikio, macho wala mabega”

Thornton amefanya kazi na Kampuni hiyo tangu mwaka 2016 na akaanza kufuga rasta mwaka 2019 lakini baadaye akahamishiwa Tawi la San Diego akitokea Ofisi ya zamani ya Florida mwaka 2020 na Boss wake akamwambia akate nywele zake ili aendane na viwango vya ofisi hiyo mpya na pia akiahidiwa kuwa kama angekata rasta basi angepandishwa cheo na kupewa nafasi nzuri zaidi.

Kampuni hiyo imesema kulikuwa na tatizo la kimawasiliano kati yao na Thornton na kusema itazipitia upya Sera zao, Thornton amesema anataka aombwe msamaha na Kampuni na iahidi kuondoa sera na masharti ya kuwapangia Watu mtindo wa maisha kazini huku akisema anaamini nafasi yake bado ipo lakini hajasema kama atarudi kuendelea na kazi.

RAIS SAMIA AWAVAA WASALITI, AVUNJA BODI TPA “WATU WA HOVYO, WANASEMA UFISADI AWAMU YANGU”

Soma na hizi

Tupia Comments