Top Stories

Ajabu la Dunia, Mama ajifungua kalunguyeye “Nimesikia uchungu”

on

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mwanamke mmoja aitwae Regina Mataba (46) Mkazi wa Sima Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu amedai kujifungua mnyama aitwae Kalunguyeye baada ya kubeba ujauzito kwa miezi minne.

Baada ya kubeba ujauzito huo ilipofika Jumapili Septemba 12 Regina amedai alihisi uchungu na kwenda chooni ambako alijifungua mnyama huyo ambae awali alionekana kama panya buku ila alimwagiwa maji ya baraka na ikagundulika kuwa ni mnyama aina ya Kalunguyeye na alikufa baada ya siku mbili.

Hata hivyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bariadi Dk. Costantine Emmanuel amesema kwenye vipimo vyote vilivyofanyika vimeonesha Mama huyo hakuwa na ujauzito ambapo pia mji wa mimba haukuonesha kama katoka kujifungua hivi karibuni, kwa upande mwingine mmoja wa Viongozi wa dini kutoka Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Luka Katekista Ibrahimu Gibayu aliongoza ibada fupi ya kukiteketeza kwa moto kiumbe hicho.

WALIOFARIKI AJALI YA MWENDOKASI, FAMILIA YATOA TAMKO, RAFIKI ASIMULIA ALIVYOWAAGA

Tupia Comments