Wiki moja tangu kutokea kwa ajali ya New Force iliyoua Watu saba na kujeruhi wengine 48 Mkoani Njombe wakati Dereva aki-overtake Darajani, leo July 02,2023, Basi jingine la Newforce lenye namba za usajili T448 DDT lilikokuwa linatokea Iringa kwenda Dar es salaam limepata ajali eneo la Mlima kitonga mara baada ya Dereva ku-ovetake Mlimani.
@AyoTV_ imeongea na RPC wa Iringa Allan Bukumbi kwa njia ya simu na amethibitisha ajali ajali na kusema hakuna majeruhi wala kifo na kwamba basi hilo lilikuwa na abiria 57 na lilipinduka mara baada ya dereva kuyapita magari mengine na kushindwa kurudi katika mstari wake na ndipo alipogonga jiwe na gari hilo kupinduka.