Michezo

Ajali ya Modisha familia yataka DNA

on

Klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini imetoa taarifa kuwa familia ya marehemu mchezaji wao Motjeka Modisha ,25, inasubiri majibu ya DNA ili kuthibitisha kama mtu aliyefia kwenye gari ya Modisha ni Modisha mwenyewe.

Sababu ya kutaka kuthibitisha hilo ni kutokana gari aina ya BMW inayoaminika kuwa ndio alikuwa akiendesha Modisha iliwaka moto na kuwa majivu kitu ambacho mwili wake haukuweza kutambulika.

Awali iliripotiwa kuwa Modisha alifariki alfajiri ya Jumapili December 13 2020 maeneo ya Kempton Park Afrika Kusini kwa gari yake kuwaka moto akiwa njiani akitokea katika maadhimisho ya miaka 50 ya club ya Mamelod Sundowns lakini familia inaripotiwa kuwa inahitaji kujiridhisha zaidi.

Soma na hizi

Tupia Comments