Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM chini ya Kamanda Jumanne Muliro wametoa taarifa rasmi ya ajali ya basi la Mwendokasi na gari dogo iliyotokea February 22,2023.
Muliro amesema majeruhi waliopo Hospital ni wanne, Watatu ni waliokuwa kwenye gari ndogo iliyosababisha ajali ambao ni Dereva na abiria wake wawili na wamelazwa Muhimbili, na mmoja ni Mtembea kwa miguu alielazwa Taasisi ya Mifupa MOI.
“Chanzo kikubwa cha ajali hii ni uzembe na kutojali kwa dereva wa gari dogo ambaye alijarinu kukatisha barabara ile ya mwendokasi bila kuchukua tahadhari wakati huo Mwendokasi ikiwa kwenye barabara yake” Muliro