“Asubuhi tutakuwa na zoezi la kunyanyua mabehewa tutahakiki kuwa hatuna masalia asubuhi, tumepata vifo vitatu na Treni ilikuwa na abiria 720 kwa hiyo ni wengi sana, lile eneo ambalo treni imepinduka bila SGR ilikuwa si rahisi kufika tumeingia kirahisi mabasi yamefika yamechukua Watu wote kwa pamoja”
“Kule mvua imenyesha sana inaonekana baada ya mvua kunyesha na lile eneo ni tambarare ile reli huwa inanyanyuliwa kwa hiyo inaonekana imeenda ikaosha ule msingi wote reli ikabaki pekee yake kwa hiyo tuna wasiwasi reli ilizidiwa ndio maana ikaanguka”-Dkt. Binilith Mahenge Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.