Habari zilizotufikia kutoka Mwanga Mkoani Kilimanjaro zinasema kuna ajali mbaya imetokea maeneo ya Mwanga wakati basi la kampuni ya Mbazi Travellers lililokua likitokea Arusha kuelekea Dar es salaam kupinduka.
Taarifa kutoka kwa ripota wangu wa nguvu zinasema ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo kujaribu kulipita basi jingine huku kukiwa hakuna mtu aliyepoteza maisha lakini inasemekana kuna idadi kubwa ya majeruhi ambao walikimbizwa katika hospitali ya KCMC Moshi.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook