Ajali

Nahodha wa Simba Jonas Mkude amepata ajali

on

Siku moja baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya Simba dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Jamhuri Dodoma na Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2-1, leo May 28 nahodha wa timu hiyo Jonas Mkude ameripotiwa kupata ajali.

                                                                 Jonas Mkude

Mkude ambaye alikuwa katika gari binafsi na baadhi ya watu amepata ajali ya gari akitokea Dodoma akiwa maeneo ya Dumila mkoani Morogoro akiwahi Dar es Salaamkwa ajili ya kambi ya timu ya taifa Taifa Stars.

Kutoka Kushoto ni beki wa Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ shabiki na Said Ndemla kiungo wa Simba SC

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Mkude ameumia maeneo ya shingo na amepelekwa hospitali wakati mmoja kati ya abiria waliyokuwemo katika gari hilo akiripotiwa kupoteza maisha millardayo.com inaendelea kufuatilia taarifa hizi na itakuletea hapa.

Unaweza kutazama mahojiano ya Mkurugenzi wa SportPesa na AyoTV baada ya kuingia mkataba.

Soma na hizi

Tupia Comments