Watu 19 wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea leo Agosti 16,2022 katika eneo ya Shamwengo, Inyala Mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi mkoani, Urlich Matei amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, akieleza kuwa gari la kampuni ya Evarest Frech Ltd likiwa na kontena la mchanga lilifeli breki na kuligonga basi la Super Rojas lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe.