Ajali

VIDEO: Wazanzibari wasimulia upepo mkali uliowakumba wiki hii

on

Mapema wiki hii kuliripotiwa taarifa ya upepo mkali ambao uliyakumba baadhi ya maeneo Visiwani Zanzibar ambapo ulisababisha madhara ukiharibu nyumba za watu, mali na miundombinu.

Kutokana na ukali wa Upepo huo baadhi ya Watu walikosa pa kulala na kupoteza mali walizokuwa wanazimiliki hasa nyumba zao kubomolewa na kung’olewa mabati jambo lililowafanya kuomba msaada kwa wasamaria wema.

Ayo TV na millardayo.com zimefika Visiwani Zanzibar ambako iliweka kambi Nyarugusu katika Mkoa wa Mjini Magharibi na Wilaya ya Magharibi B na kujionea maafa yaliyosababishwa na upepo huo ambapo baadhi ya wahanga wa tukio hilo akiwemo Suleiman Ally Makame mkazi wa Nyarugusu wamesimulia namna upepo huo ulitokea na kusababisha maafa: 

>>“Tukio la Kimbunga lilitokea kweli kama majira ya saa 3:15 asubuhi…nikasikia midato mikubwa sana aina ya Radi…nikatoka kwenye kibanda kusimama nje, kutizama juu nikaona siyo Radi. Nikaona mabati yanaanza kusambaa juu yamegawika katika sehemu mbili; yaliyokuwa yanapita mbali na yaliyokuwa yanapita chini chini.” – Suleiman Ally Makame.

Kutazama zaidi unaweza kubonyeza play kwenye hii video hapa chini kupata yote waliyoyasema>>>

Mafuriko yaliyotokea DSM na kusababisha kifo cha mtu mmoja…

Soma na hizi

Tupia Comments