Michezo

Ajax kuvunja mkataba na mchezaji wake aliyekua majeruhi miezi 33

on

Club ya Ajax ya Uholanzi ikiwa  ni wiki moja tu imepita toka nyota wao Abdelhak Nouri aanze kuchezesha baadhi ya viungo vyake toka awe katika coma kwa miaka miwili na miezi 9.

Ajax imeripotiwa kuwa imesitisha mkataba na Nouri ambaye bado yupo kitandani katika majeraha ambayo aliyapata kwa kuanguka uwanjani akiitumikia timu hiyoka katika mchezo wa kirafiki.

Kwa sasa Ajax ambayo ilikuwa ikimlipa mshahara Nouri toka July 2017 kwa heshima ya kupata matatizo akiwa katika timu yao sasa imepanga kukutana na wanasheria na familia ya mchezaji huyo.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Nouri alianguka na kupoteza fahamu uwanjani July 2017 kwa tatizo la moyo (cardiac arrhythmia) katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Werder Bremen.

Wiki moja iliyopita alizinduka na fahamu kumrejea baada ya kuwa katika coma kwa miaka miwili na miezi 9, kwa mujibu wa kaka yake Nouri sasa anachezesha macho, kula na kuchezesha sura.

Soma na hizi

Tupia Comments