Mwanafunzi mmoja anapatiwa matibabu Hospitali ya Makadara Kaunti ya Mombasa nchini Kenya baada ya kupigwa na Walimu wake kisa kula chapati tano wakati alipaswa kula chapati moja aliyopewa, inadaiwa miongoni mwa chapati alizokula kuna za Mwalimu wake.
Mama wa Mtoto huyo anasema “Madam akaniambia hii ni kesi kidogo, nikiangalia kile kinasemekana ni kitu kidogo, Mtoto wangu kusimama hawezi, mpaka ashikiliwe, ukimwangalia mgongoni ni kama a amechomwa ana alama kila mahali ya vidonda”
“Walimu walimpiga wakapumzika wakamwambia tukutane tena baadaye na walipompiga hawakunijulisha Mimi Mzazi, hakuna kitu inaumiza kama nikuleetee Mtoto akiwa mzima alafu unirejeshee akiwa mlemavu, sijui kama atapona maana figo yake moja imeathirika, imesemekana ataanzishiwa dialysis wakati Mimi nilipeleka Mtoto Shuleni akiwa mzima”
Inadaiwa baada ya Walimu kumpiga waliona haitoshi wakawaambiwa na Wanafunzi wenzake wampige na alipozidiwa wakashindwa kumpeleka Hospitali na kupambana kumpa huduma ya kwanza Shuleni hadi Wazazi walipopewa taarifa, kwa sasa Mtoto anaendelea na matibabu ambapo licha ya kujeruhiwa amepata pia shida kwenye figo yake na sehemu zake za siri pia zina majeraha, Serikali imeifunga Shule hiyo kwa kutokidhi masharti ya usajili kufuatia tukio hilo la kumjeruhi Mtoto.