Top Stories

Ajifungua salama ndani ya ndege iliyokua ikisafiri kutoka Ghana kwenda Marekani

on

Mwanamke mmoja amejifungua salama ndani ya Ndege iliyokua ikisafiri kutoka Ghana, Afrika kwenda Marekani akiwa ndani ya Ndege ya United Airlines Flight 997 ambayo safari yake ni saa 11 angani.

Baada ya kukaa angani kwa saa sita Mwanamke huyo alisikia uchungu ikamlazimu Rubani atangaze kama kuna Abiria yeyote Daktari ambapo bahari nzuri akapatikana na kumsaidia Mwanamke huyo kujifungua salama.

“Wahudumu wetu walichukua hatua haraka, wakasaidia Wataalamu wa matibabu ndani ya ndege na kuhakikisha kila Mtu anakaa salama wakati wote wa ndege na tulifurahi sana kuona ndege ikitua ikiwa na Abiria mmoja wa ziada, haswa mrembo“- Taarifa ya United Airlines imesema.

LULU DIVA AJITOKEZA NA KUANDIKA MAZITO MSIBA WA MAMA YAKE ‘NI PIGO ZITO, NIMEONDOKEWA’

 

Soma na hizi

Tupia Comments