Kijana mmoja anayejukikana kwa jina la Elirehema Ernest anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 31 mkazi wa kijiji cha Oldadai kata,ya Sokone 11 Wilayani Arumeru Mkoani Arusha amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia mkanda wa begi huku akiwa amevaa gauni na viatu vya mpenz wake nakuacha ujumbe kuwa mpenzi wake wa chuo asisumbuliwe kwa kuwa hausiki na maamuzi yake
Lomayani Kivuyo Mwenyekiti wa kijiji cha Oldadai amesema kuwa kijana huyo alikuwa na ugomvi na mpenzi wake huyo anayesoma chuo jijini Dar es Salaam na siku moja kabla ya kujinyonga alimpigia baba wa marehemu nakumtaka amrudishie funguo la duka la biashara walilokuwa wakiuza vinywaji katika eneo la Ngulelo
“Ujumbe unahusiana na mpenzi wake ambaye alikuwa anaishi naye kimahusiano na walikuwa wanashirikiana kwa pamoja,ujumbe huo ni kwamba asisumbuliwe binti yule ambaye anaitwa Bahati kwa sababu hajahusika na jambo lolote,amemtakia heri ya maisha”