Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema Rebecca Benjamini Mkazi wa Kata ya Izunya Wilaya ya Nyang’hwale mwenye umri wa miaka 17 amefariki dunia kwa kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo baada ya kuwa anaachwa kila anapoolewa “Ameachika mara tatu kwenye ndoa”
Mwaibambe amesema hayo alipokutana na Kamati ya Amani na Maadili ya Mkoa wa Geita, ambapo amesema chanzo cha kifo cha Rebecca ni msongo wa mawazo ambao ulikuwa ukisababishwa na yeye kuolewa na kuachika mara kwa mara.
“Rebecca amefariki dunia baada ya kujinyonga hadi kupoteza maisha kwa kutumia kamba iliyosukwa kwa chandarua kwenye kenchi ya nyumba yake, chanzo alikuwa akilalamika kwamba kwanini kila akiolewa anaachika na tayari alikuwa ameshaachika mara tatu”
Baadhi ya Viongozi wa Dini aliokutana nao leo kutoka katika Madhehebu mbalimbali ili kutokomeza matukio ya Watu kuua na kujiua, wamesema Wananchi wanatakiwa kuwa na hofu ya Mungu.