Top Stories

Ajiua kwa kujimwagia Petrol na kujichoma

on

Hashimu Selemani maarufu Chikwisu mkazi wa Mtaa wa Julia Newala Mjini Mkoani Mtwara amefariki dunia baada ya kujimwagia mafuta ya petrol mwilini na kujichoma moto chanzo kikitajwa kuwa ni ugomvi wa kimapenzi na Mkewe.

Mtoto wa Marehemu Msafiri Hashimu amesema chanzo cha Baba yake kujiua ni baada ya kumfumania Mkewe na Mchepuko wiki moja iliyopita ambapo baada ya tukio hilo hakuwa sawa hadi kufikia kujichoma moto.

“Hashimu alifikishwa Hospitali akiwa ameungua kwa kiasi kikubwa kuanzia kichwani mpaka maeneo ya tumboni, tumepambana kumpatia matibabu lakini kwa bahati mbaya amefariki” – Swaumu Zuberi, Daktari Ndanda Hospital

Mwenyekiti wa Mtaa wa Julia Abdalah Mpende amesema Wanandoa hao walishawahi kufika kwake baada ya Mwanaume kumfumania Mkewe ambapo waliumaliza ugomvi huo na hakuwafuatilia tena hadi aliposikia Mume kajiungza “Mke wa Marehemu ametoweka na anatafutwa na Polisi”.

MAGUFULI AMVAA KITILA MKUMBO HADHARANI “NILIKOSEA KUCHAGUA VIONGOZI, KWAKO WANAFUNZI WANAKAA CHINI”

Soma na hizi

Tupia Comments