Kutokea Dar es salaam nakukutanisha na Lilian Mmari, mzaliwa wa Sanya juu Siha mkoani Kilimanjaro ambae ameamua kujipa maua yake mwenyewe kwa kujipa zawadi ya Jumba la kifahari lenye kila kitu ndani kwenye siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake July 24, 2024 wakati akitimiza umri (39).
Akiongea na @Ayo TV, nyumbani kwake Mbezi ya juu Jijini Dar es salaam Lilian anasimulia kwamba hakuanza kirahisi hadi leo hii kuona anaweza kujizawadia jumba la kifahari lenye ghorofa moja, hakuwahi kuamini kwenye upande wa kushindwa licha ya kuanza na mtaji wa laki mbili tu, akichukua bidhaa soko la Kariakoo na kuzitembeza wakati huo akiwa Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara CBE, Dar es salaam.
Lilian akiwa ni msomi wa Shahada ya Masoko, hakuwahi kutamani kutafuta ajira kwani ajira za ma-ofisini aliamini huwenda zitamchelewesha kufikia ndoto zake na kusimama upande wa kujiajiri.
@Ayo TV, imemtembelea Lilian nyumbani kwake na amekubali kutuonesha kila kona ya jumba lake, Karibu usikie mengi kutoka kwa Mwana Mama aliyejizawadia jumba la kifahari kwenye kumbukumbu yake ya kuzaliwa.
#MillardAyoUPDATES