Mix

HUZUNI: Watu wengine watano wamefariki Arusha

on

Ikiwa bado Watanzania wapo kwenye majonzi ya msiba wa watu 32 kwenye ajali ya basi dogo la shule Karatu Arusha, vifo vingine vya mkupuo vimetokea kwa watu watano waliokua ndani ya nyumba.

Watu hawa watano wamefariki baada ya kuangukiwa na mti kwenye kijiji cha Ngiresi kilichopo Kata ya Sokoni mkoani Arusha ambapo kamanda wa Polisi Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Amesema imetokea usiku wa kuamkia leo May 9, 2017 baada ya mti kuangukia kwenye nyumba iliyokua jirani ambapo chanzo ni mvua na upepo mkali.

Unaweza kumsikiliza Kamanda kwa ku-play hapa chini…

VIDEO: Maombolezo ya kitaifa ya wanafunzi wa Lucky Vicent, Arusha

VIDEO: Kali nyingine ya Kagera, Mchungaji aoa Mke wa Muumini

Soma na hizi

Tupia Comments