Ajali

PICHA 5: Imenifikia taarifa ya Gari kuzama Baharini April 20 2016….

on

February 2016 iliripotiwa ripoti ya kuzima injini ya Pantoni na kuleta tafrani kwa abiria, sasa ni takribani miezi miwili tangu tukio hilo litokee. Daraja la Nyerere ‘Kigamboni’ lililozinduliwa jana limeonekana msaada mkubwa kwa wakazi wa Dar es salaam hasa Kigamboni.

Usiku wa siku ambayo Daraja lilizinduliwa April 19 2016 imetolewa taarifa ya gari moja aina Toyota Hiace yenye namba za usajili T271 CRG  kuserereka kutoka kwenye pantoni na kuzama baharini. Pantoni hilo lilikuwa likivuka kutoka Posta kuelekea Kigamboni Alfajiri ya April 20 2016.

Watu waliosadikiwa kuwa ndani ya gari hilo ni wawili au watatu na mpaka sasa mtu mmoja ameokolewa na Jeshi la zimamoto na uokoaji. Kati ya watu walikuwamo ndani ya gari hilo ni dada wa Brown Mwakalago ambaye ameyazungumza haya……

>>>tulikuwa tunatoka msibani Mbeya, yule dada yangu aliyekuwa mle ndani ya gari alikuwa amepanda kwa sababu alikuwa anajisikia vibaya, tulipokuwa tumekaa pembeni tukaona gari linaserereka kwenda mbele na kwenda kwenye maji kwa hiyo dada yangu hajaonekana mpaka sasa hivi’

Pia Meya wa Jiji la Dar es salaam,  Isaya Mwita amefika na kulizungumzia kuwa ….>>>’uwenda zile lock za kule nyuma hawakuzifunga, huenda ni uzembe kwa hiyo tunangojea ripoti huko ndani tujue nini kilichojiri jana usiku’

kiongozi wa uokoaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Abdu Swala amesema …….>>>‘tulifanikiwa kutoa mwili mmoja na bado tunaendelea kutafuta chombo chenyewe na mtu ambayo inasemekana walikuwemo watu wawili hadi watatu taarifa kamili bado hazijatolewa’

.

.

.

.

IMG-20160420-WA0014 IMG-20160420-WA0015 IMG-20160420-WA0016

ULIIKOSA YA SHUHUDA WA PANTONI LA KIGAMBONI INJINI ILIVYOZIMA KATIKAKATI?  ANAGALIA VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments