Mwanaume mmoja alitambiliwa kama Mark Muffle yupo chini ya ulinzi baada ya kukamatwa na begi lililokuwa na kilipuzi lilipatikana kwenye mizigo iliyokaguliwa wakati wa ukaguzi wa kawaida kwenye uwanja wa ndege wa Pennsylvania.
“Wakati wa ukaguzi wa mara kwa mara wa mizigo iliyokaguliwa, koti kifaa cha ukaguzi kilipiga kelele kuashiria hakikuwa kitu salama ndani yake na wakala wa TSA akakagua ili kuona kilichokuwa ndani kilionekana kutiliwa shaka na kiliaminika kuwa kilipuzi cha moja kwa moja,” shirika hilo lilisema.
malalamiko ya jinai yaliyowasilishwa na Askari Maalum wa FBI Eddie Garcia ni kuwa mshukiwa anashtakiwa kwa kosa la kujaribu kuweka, au kupandanda na kilipuzi au kifaa cha kuwasha moto kwenye ndege.
Garcia alisema katika jalada hilo kwamba kulipatikana kilipuzi kingine kilichokuwamo kwenye mfuko wa koti kwenye begi hilo.
“Ina aina ya punjepunje ya poda iliyofichwa ndani ya karatasi na kitambaa ambayo mara nyingi hupatikana katika fataki”.
Wakati mamlaka ilipopata kilipuzi kwenye mzigo wake, Muffley aliarifiwa na kutakiwa kufika kwenye dawati la usalama /mamlaka husika japo dakika tano baadaye alionekana kwenye kamera za uwanja wa ndege akitoroka.
Baada ya upelelezi kufahamu mwanaume huyo alipo walimkamata muffle nyumbani kwake Jumatatu usiku, kulingana na taarifa na yuko kizuizini toka Jumatano usiku na atafikishwa mahakamani siku ya leo alasiri kwa sababu ya kesi kusikilizwa.
Haijulikani ikiwa Muffley ana wakili anayeweza kutoa maoni kwa niaba yake.