Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Goa Amalila Mwanguli 27 Amekamatwa katika Hifadhi ya Taifa Ruaha na Askari wa hifadhi hiyo huku akiwa na Kichwa cha Chatu Pamoja na Mkia wake , Samaki wabichi pamoja na Silaha za Jadi ikiwemo panga.
Akizungumza na AyoTv leo Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole mei’ngataki amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa na Askari wa Hifadhi wakati wa Doria katika Eneo la Mwanjulwa huku wenzake kukimbia na lakini Mtuhumiwa Goa alivyohojiwa kuwa anapeleka wapi chatu alisema kuwa Huwa wanampika na kula nyama yake
“ tuliweza kumuhoji natulishangazwa kuwa huyu mtu anapeleka wapi Chatu kwanini wanauwa chatu , akawa anatueleza kwamba ni wanakula nyama yake huwa wanamchuna ngozi na kumpika na kula nyama na tulipomuhoji zaidi kuhusu kichwa cha chatu na mkia alisema huwa zinatumika kwenye imani za Kishirikina ambazo sisi atuzifahamu ninini “ Amesema Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha
Godwell Ameendelea kusema “ wavuvi haramu huingia hifadhini kufanya uvuvi haramu wanauwa wanyama wengi sana ambao huwa katika mazingira ya Samaki kwa maana ya maji akiwemo huyu chatu kwa kutumia nyavu na wanyama wengi sana watambaao hunaswa na nyavu zao hivyo madhara makubwa ya uvuvi haramu ni kuendelea kuuwa wanyama wengi ambao wako katika mazingira ya Maji “ Amesema Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha
Mamlaka ya hifadhi ya Ruaha imeendelea kuonya dhidi ya vitendo vya ujangili zikisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitazidi kuchukuliwa dhidi ya yeyote anayekiuka sheria za Hifadhi hiyo .