Habari za Mastaa

Kumbe Akon kawahi kufika Kenya mara tano? Mipango ya collabo je?

on

Akon-Net-Worth

Huenda Kenya ikawa na bahati ya kutembelewa na staa huyu mara nyingi zaidi kuliko nchi nyingine Afrika.. Akon amesema amewahi kutembelea Kenya mara tano.

Jamaa anafanya muziki wake Marekani, ila ana asili ya Senegal.. anaona labda wasanii wa Kenya hawajaitumia vizuri nafasi yake mara zote ambazo ametembelea Kenya kwa kuwa hajawahi kufanya collabo na msanii yoyote wa nchi hiyo wala hakuna aliyeuomba kufanya nae hivyo.

Star huyo ambaye ni mmiliki wa lebo ya muziki ya Kon Live aliwahi kufanya kazi na mastaa wakubwa duniani kama marehemu Michael Jackson na Whitney Houston50 Cent, Lionel Richie na wengine.

Akon amesema alichokiona ni kama wasanii wa nchi hiyo hawakuwa na utayari kufanya nae collabo, “I have come here mostly for my projects about solar power solutions for slums, but it is unfortunate that I have not had time to work with a Kenyan artiste“– Akon.

Kaa karibu na millardayo.com nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments