AyoTV

AUDIO: Jeshi la polisi Mwanza limemkamata askari feki

on

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Ahmed Gabo umri wa 22 kwa tuhuma za kukutwa amevaa sare za jeshi la Polisi kinyume na sheria, Gabo anadaiwa kuiba sare hizo, millardayo.com na Ayo TV imempata Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Mwanza, Ahmed Msangi na amezungumza haya………

>>>‘Kwa jinsi alivyovaa sare  za Polisi kofia, mkanda mpaka viatu na hali aliyokuwa nayo ni kinyume na askari anavyotakiwa awe na maadili aliyokuwa anaonyesha sio ya Kipolisi’

>>>‘Tumemhoji kwa haraka na amekiri ni kweli hizi sare sio zake na wala hajawahi kuwa kwenye mafunzo yeyote ya kijeshi bali ameiba begi la muumini ambae alikuwa anaswali katika msikiti siku nne zilizopita huyu muumini ni  Askari Polisi wa hapa mkoani;- Ahmed Msangi

Kumsikiliza kamanda Ahmed Msangi unaweza kubonyeza play hapa chini

ULIKOSA MAAGIZO YA RAIS MAGUFULI KWA TCU KUHUSU ONGEZEKO LA VYUO VIKUU? UNANAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI 

Soma na hizi

Tupia Comments