Klabu ya Al Hilal ya ligi kuu nchini Saudi Arabia imemfuta jina mshambuliaji wa Brazi Neymar Jr kwenye mipango yao ya msimu huu ya kuwania taji la Saudi Pro League.
Kocha wa Al Hilal Jorge Jesus alisema;”Ney hatasajiliwa, lakini anaweza kushiriki Ligi ya Mabingwa ya Asia”.
“Yeye ni mchezaji wa kiwango cha ulimwengu. Lakini kimwili, Neymar Jr hawezi tena kucheza kwa kiwango ambacho sisi sote tumezoea kuona”.
“Bado yuko chini ya mkataba na Al Hilal na inaweza kuwa juu yake kuamua mustakabali wake, pia juu ya utawala”.
Klabu ya Chicago Fire ya Marekani walimwendea Neymar kwaajili ya kumsajili lakini bado hajakubaliana nao chochote.