Habari za Mastaa

Album ya marehemu Pop Smoke ‘Faith’ yakamata namba 1 charts za Billboard

on

Japo Marehemu Pop Smoke amefariki lakini kazi zake ziko uhai na zinaendelea kufanya vizuri kwenye soko la Muziki, Uongozi unaosimamia kazi za Rapper huyo baada ya kuachia album yake mpya iitwayo ‘Faith‘ hivi karibuni imefanikiwa kukamata nafasi ya kwanza kwenye charts za Billboard 200.

Album hiyo iliyoachiwa mwezi Julai 16, 2021 unaambiwa imeuza jumla ya nakala 88,000 kwahiyo Marehemu Pop Smoke anakuwa na jumla ya album mbili  ikiwemo Shoot for the Stars Aim for the moon iliyoachiwa mwaka 2020 ambayo nayo bado inapeta katika chats mbalimbali.

MWIJAKU ANAITAKA KAZI YA MANARA SIMBA ” SIFA NINAZO”

 

Soma na hizi

Tupia Comments