Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama amepewa tuzo ya Heshima na Chama cha Muziki wa Injili nchini (CHAMUITA) kama Muandaaji Bora wa matamasha ya nyimbo za Injili muda wote kuinua na kusapoti muziki huo pamoja kusapoti wasanii wadogo
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo kutoka kwa Rais wa chama muziki wa injili Tanzania CHAMUITA Ndugu Ado November Msama amesema kuwa anashukuru kwa tuzo ya heshima aliyopewa na anahamini itazidi kumpa chachu ya kuendeleza na kuzidi kuinua muziki huo.
“Nimetoka mbali nimefanya kazi nyingi sana nilikuwa dereva, nimebeba mizigo Kariakoo lakini kubwa ni kutangaza kazi za waimbaji wa nyimbo za Injili, nashukuru kwa kutambua Mchango na juhudi zangu katika kutangaza muziki wa Injili.
“Nitaendelea kusapoti Muziki wa Injili na kuzidi kuinua na kuwapa ushirikiano wasanii wachanga wa muziki huo kama nilivyoshirikiana na kuwasapati waimbaji wakubwa hapa nchini na sasa nitahakikisha tunawatambulisha kina Rose Muhando, Boniface Mwaitege na Bahati Bukuku wengine.”amesema Msama
Pia ameongeza kuwa tuzo aliyopewa sio ya Msama peke yake bali ni tuzo ya mashabiki wote na wapenzi wa muziki wa Injili nchini na nje ya nchini.
“Niwahakikishie watanzania kujiandaa na Tamasha la Pasaka litafanyika kwa kishindo na kama mnavyoona huu ni mwanzo na naendea kuupambania Muziki wa Kumtukuza Mungu.
Aidha amewataka wasanii wa nyimbo za Injili kujitofautisha na wasanii wa Bongo fleva kwa kuwa wao wanamsifu Mungu na kuacha tamaa ya vitu vya duniani wamtumikie Mungu.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania Ado Novemba amesema kuwa ni kwa Muda mrefu tumekuwa tukifanya kazi na Msama Leo tumetambua Mchango wake muhimu katika Tasnia hiyo.
Miongoni mwa wasanii waliopata tuzo hizo za heshima za kuupigania muziki huo wa Injili ni pamoja na Msanii Malkia wa nyimbo za Injili Rose Muhando pamoja na Cosmas Chidumule aliyekuwa akiimba muziki wa dansi na kuamia kumrudia Mungu na sasa anaimba wimbo wa Injili.