Top Stories

Alichofanya Dada alipomfuma mpenzi wake akinywa ARVs

on

Gazeti la Daily Monitor la Uganda, limeripoti kuwa Mwanamke mmoja katika Wilaya ya Hoima, Uganda anashikiliwa na Polisi akidaiwa kumuua mpenzi wake Emmanuel Tumusiime kwa kumpiga na shoka kichwani baada ya kumfuma akimeza dawa za kupunguza makali ya Virusi Vya Ukimwi (ARVs)

Msemaji wa Polisi Hoima Julius Hakiza amesema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa Emmanuel mwenye umri wa miaka 35 alishambuliwa mpaka kuuawa nyumbani kwake katika Mji wa Kigorobya majira ya saa kumi na mbili jioni.

Unaambiwa alipogundua kwamba Mpenzi wake amefariki, Mwanamke huyo alifunga nyumba na kupanda Bodaboda mpaka kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Hoima na kuripoti kuwa amemuua Mpenzi wake.

Hakiza ametoa wito kwa Watu wenye Virusi Vya UKIMWI kuwapa taarifa Wapenzi wao ili wawe wanahudhuria pamoja Hospitali na kupewa ushauri nasaha kwani kuwa na UKIMWI sio mwisho wa Maisha.

INJINIA HUYU ASUKUMIWA NDANI “WAZIRI UTAPATA BP UKIONA BANDA, LIMEJENGWA KWA MILIONI 100”

Soma na hizi

Tupia Comments