Habari za Mastaa

Alichofanya Davido kwa Bilioni 1 alizokusanya siku ya birthday

on

Staa wa wa muziki wa Nigeria  David Adedeji Adeleke, (Davido) ametoa orodha ya vituo vya yatima vya nchini Nigeria ambavyo alivipatia jumla ya Naira 250 Million ambazo ni 1389082546 za Kitanzania.

Taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa Twitter Davido – alifichua kuwa alitimiza ahadi yake ya mwaka 2021, alipopokea Mamilioni ya Naira katika kipindi cha saa 72 baada ya kuushirikisha umma akaunti yake ya benki kwenye mitandao ya kijamii wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa kwake.

“Kama nilivyoahidi, kamati ya wanaume watano ya usamabazaji wa pesa iliwekwa. Tangu ilipozinduliwa, wajumbe wa kamati hii wamefanya kazi bila kuchoka kuhakikisha wanakusanya majina na taarifa zilizopo na kuhakikisha vituo vya yatima. Ninafuraha kutangaza kuwa utoaji wa pesa umekamilika ,” Davido

“Hadi sasa jumla ya Naira 250,000,000 zimetolewa katika vituo 292 vya yatima,” ilifichua taarifa yjake, na kuongeza kuwa, “Katika moyo wa kuwa na uwazi nilidhani ni busara kuwafahamisha wanaoniunga mkono, mashabiki, marafiki na familia yaliyofikiwa kuhusiana na hili.” Davido

“UKIMUIBIA HUYU MZEE UNAZIKWA, MAZIWA YA NYOKA” KIKONGWE ZANZIBAR ASIMULIA MAKUBWA

Soma na hizi

Tupia Comments