Rapper wa kundi la Weusi Joh Makini ametumia ukurasa wake wa Facebook kuandika kuhusu Lord Eyez ambae ni mwanachama wa kampuni ya WEUSI ambae amesimamishwa kazi kwenye kampuni hiyo siku kadhaa tu baada ya kuingia kwenye headlines za kushikiliwa na Polisi Arusha kwa tuhuma za kuvunja gari na kuiba laptop iliyokuwemo ndani.
Hata hivyo Joh Makini alituma msg kwa millardayo.com na kutoa ufafanuzi wa hii ishu kwa kusema ‘Lord Eyez hajafukuzwa wala kutengwa na WEUSI kama wengi mnavyofikiri bali tunampa muda huku tukishirikiana nae kumaliza matatizo yake na atakapokua sawa atarudi kazini kama kawaida’