Mix

Alichosema Cristiano Ronaldo baada ya Falcao kuhamia Man United

on

IMG_6950.JPG

Usiku wa jana klabu ya Manchester United ilikamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao kwa mkopo.

Falcao ambaye alikuwa akiwindwa na vilabu vya Arsenal na Man City amejiunga na Man U akitokea klabu ya Monaco ambayo alijiunga nayo akitokea Atletico Madrid.

Usajili wa mchezaji umezungumzia na watu wengi mmoja wao ni mchezaji bora wa ulaya na dunia – Cristiano Ronaldo.

Akiongea jijini Madrid Ronaldo alisema: ‘Falcao ni mchezaji mzuri sana, nadhani Manchester United wamefanya jambo zuri kumsajili. Sidhani kabisa kama ni mchezaji asiyewafaa, ni mchezaji wa daraja la dunia na hivyo naamini huu usajili mzuri.”

Tupia Comments