Michezo

Alichosema Dwight Yorke juu ya timu 3 ambazo Man United inaweza kuzifunga robo fainali ulaya

on

7-ngoi-sao-tung-hoi-tiec-vi-quyet-dinh-chia-tay-Man-UtdBaada ya ushindi wa jana wa 3-0 dhidi ya Olympiakos ambao uliwapeleka Manchester United katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya, watu wengi hasa mashabiki wa Man United wamekuwa na shauku ya kutaka kujua timu ambayo watapangwa nayo kucheza nayo robo fainali ya Champions League hapo kesho pindi ratiba itakapopangwa.

Wakati mamilioni ya mashabiki wa timu hiyo wakisubiri ratiba, gwiji wa soka na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Dwight Yorke amezitaja timu 3 ambazo kama ikitokea moja wapo ikapangwa kucheza na United katika hatua ijayo ya ligi ya mabingwa ulaya, basi timu yake ya zamani itapata matokeo chanya.

Yorke amezitaja timu za Atletico Madrid, Borrusia Dortmund na PSG – kwamba kati ya timu yoyote kati hizo, ikitokea mojawapo imepangwa kucheza na United basi klabu yake ya zamani itapata matokeo ya ushindi na kwenda kucheza hatua ya nusu fainali ya Champions league.

Pia amezitaja Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich kuwa ndio timu ambazo asingependa wakipangwa nazo katika hatua ijayo ya michuano hiyo.

VIDEO ZA YORKE AKIONGELEA SUALA HILO

Tupia Comments