Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Alichosema kocha mpya wa Man United kuhusu Mourinho kumuonea wivu

on

article-2633169-1E05E92000000578-923_636x454

Masaa takribani 24 tangu alipotangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal amefunguka na kusema mwanafunzi wake na msaidizi wake wa zamani kwenye klabu ya FC Barcelona Jose Mourinho ndio alikuwa mtu wa kwanza kumpongeza kwa kupata Old Trafford.

Van Gaal mwenye miaka 62 alitajwa rasmi kuwa mrithi wa David Moyes jana, na akiongea na radio ya Uholanzi alisema kwamba kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikuwa mtu wa kwanza kumtumia message kumpongeza huku akimuambia kwamba anamuonea wivu kwa kazi mpya na vilabu vingine alivyofundisha kama Barcelona, Bayern Munich Ajax na timu ya taifa ya Holland.

Van Gaal anatarajiwa kuanza kazi United mara baada ya kombe la dunia.

Tupia Comments