Mix

Alichosema Nemanja Vidic baada ya kutangaza kuondoka Manchester United.

on

115865491_football_356415c

Nahodha wa klabu ya Manchester United Nemanja Vidic amethibitisha rasmi kwamba ataondoka Manchester United baada ya msimu wa huu kuisha.

Katika taarifa yake aliyotoa kwa mtandao rasmi wa ManUtd.com, beki huyo kutoka Serbia alisemathe: “Ni mwaka wa mwisho wa mkataba wangu na nimekuwa na miaka nane mizuri nikiwa hapa. Muda wangu katika klabu hii kubwa siku zote utabaki kuwa kumbukumbu yangu zaidi katika maisha yangu ya soka.

“Sikuwahi kufikiria kama ningeshinda makombe 15 na kwa hakika sitousahau usiku ule mkubwa jijini Moscow, kumbukumbu zile nitaishi nazo milele. Hata hivyo, nimefikia uamuzi kwamba nitaondoka klabuni mwishoni mwa msimu huu. Nataka kujipa changamoto mpya kwa mara nyingine na kujaribu kufanya vizuri zaidi katika miaka ijayo.

“Sifikirii kuendelea kubakia England kwa sababu klabu pekee ambayo nilitaka kuichezea nchi hii ni Manchester United na nilipata bahati kubwa ya kuwa sehemu ya klabu hii kwa miaka mingi. Nina machaguo kadhaa na nitachagua chaguo la timu nzuri kwangu na familia yangu.

“Kwa sasa nitaweka umakini na jitihada zangu zote katika kuichezea Manchester United na kujituma kwa kila hali mpaka mwisho wa msimu.Natumaini taarifa hii inatosha kuachwa kusambaza tetesi zozote kuhusu hatma yangu.”

Tupia Comments