Premier Bet
TMDA Ad

Mix

VIDEO: Rais wa TFF baada ya kuombwa kutowatumia Diamond na Alikiba tena

on

Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF leo June 2 2017 mbele ya waandishi wa habari ametangaza kuwashukuru wote waliyokuwa wanaisapoti Serengeti Boys na kuichangia licha ya kutolewa katika mashindano ya AFCON U-17 kwa kanuni ya head to head na Niger.

Baada ya kushukuru watanzanzania na kueleza mipango yao kwa vijana wa Serengeti Boys, kuna mmoja kati ya waandishi aliuliza swali na kumuomba Rais wa TFF Jamal Malinzi asiwatumie tena Diamond na Alikiba kutokana na kutokuwa wazalendo.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mbunge wa Mtama Nape Nnauye wakati akiwa waziri wa michezo aliunda kamati ya uhamasishaji kuhusiana na Serengeti Boys kushiriki AFCON miongoni mwa waliyokuwemo katika kamati hiyo ni Diamond na Alikiba.
Baadae Alikiba na Diamond tulisikia kuwa walikataa kuimba wimbo wa pamoja wa kuhamasisha watanzania kuisapoti Serengeti Boys kwa tofauti zao binafsi “Naomba nisiongee chochote kuhusu Diamond na Alikiba naomba sana mimi nashukuru tu ni wenzetu walichaguliwa kuingia katika kamati ya uhamasishaji ya Serengeti Boys basi mimi niishie kuwashukuru tu” 

VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera

Soma na hizi

Tupia Comments