Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuua Kilambo Nyasairo (44) mkazi wa Chanika mkoani Dar es Salaam kwa tuhuma za ujambazi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum DSM, Camillius Wambura amesema jana saa tano usiku mtuhumiwa huyo alikamatwa na baada ya kuhojiwa alikiri kujihusika na ujambazi na anamiliki silaha.
Amebainisha kuwa baada ya kupekuliwa aliwapeleka Polisi kuwaonyesha alipoifukia silaha lakini wakati Askari wanachimba kuitoa, mtuhumiwa alianza kukimbia kuelekea kwenye maporomoko ya kingo za Bahari ya Hindi.
“Askari walipiga risasi hewani ili kumuonya asimame lakini hakutii aliendelea kukimbia na kusababisha askari kumpiga risasi mguu wa kulia akaanguka chini.” Wambura
“Askari waliendelea kuchimba eneo aliloonyesha na kufanikiwa kuipata bunduki aina ya S/GUN yenye namba S/NO.006074010/CAR 0009,” Wambura