Mwanasiasa mkongwe na mwasisi wa Mapinduzi Zanzibar, Hassan Nassor Moyo amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mkoani Tanga.
Mzee Moyo ambaye pia ni Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar.
Aliratibu Maridhiano ya Zanzibar ya Novemba 5, 2009 yaliyowakutanisha Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Aman Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad katika kutafuta mbinu ya kuondoa tofauti iliyokuwepo.
Mzee Moyo alikuwa mwanachama wa Chama cha Afro Shirazi (ASP) tangu kilipoanzishwa Februari 5, 1957 baadaye Februari 5, 1977 akajiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa na kadi namba 7.