fB insta twitter

Alichokiandika Alikiba kwa wanaomponda Wizkid

on

Baada ya headlines za Alikiba kutangazwa mshindi wa MTV EMA kama Best African act zinazidi kuchukuwa nafasi kila kukicha licha ya Alikiba kutangazwa mshindi na kuhaidiwa kupewa tuzo yake, kumekuwa na comment mbaya za watu kwa Wizkid aliyepewa tuzo hiyo kimakosa.

Alikiba ameziona comment zinazomtusi na kumponda Wizkid kuhusiana na kunyang’anywa tuzo hiyo , Alikiba ameamua kufunguka na kuandika maneno haya kwenye ukurasa wake wa Instagram baada yakuona maneno yanazidi kwa staa wa Nigeria Wizkid. 

>>>’Sijafurahishwa na ninachokiona kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii, ninamkubali sana wizkid kama msanii mwenzangu na kama mshabiki pia. Nimesikitishwa sana na kushtushwa kuona watu wakimdhihaki Wizkid kwa maneno yasiofaa na matusi, nataka kuwa muwazi tu naamini kuwa haya maneno yakijinga na yasiyofaa hayahusishi na hayajatoka kwa mashabiki wangu wa kweli kwasababu nafahamu wamekuwa wakijua jinsi gani namkubali Wizkid.

usizamishwe na maneno ya mahater bro, hongera sana kwa kuwa mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwako, upendo wa dhati kutoka kwa mashabiki wangu wa kweli na nchi ya Tanzania pamoja#KingKiba’

kiba-mavi

VIDEO: MTV EMA kuichukua tuzo kwa Wizkid na kumpa Alikiba

Soma na hizi

Tupia Comments