Michezo

Duniani wawili wawili? unavyoona hawa wanafanana na Rooney, C. Ronaldo na Messi?

on

Kwa upande wa Tanzania tumezoea kuona team ya XXL ya Clouds FM kuandaa show ya After School Bash kwa ajili ya wanafunzi kuenjoy baada ya kupata muda wa kupumzika kutoka shule au chuo, na huwa kuna time watu waliofanana na mastaa hujitokeza kama sehemu ya burudani, sasa leo naomba nikusogezee hawa jamaa wanaotajwa kufanana na mastaa wa soka.

1- Cristiano Ronaldo anafananishwa na Gokmen Akdogan

Gokmen Akdogan huyu ni mshikaji kutoka Uturuki anatajwa kufanana sana na Cristiano Ronaldo, jamaa ana umri wa miaka 23 na amekuwa akipiga pesa nyingi kutokana tu na kufananishwa na Ronaldo, wanasema amekuwa akisaini autographs na wakati mwingine kulipwa kwa kutokea kwenye matukio mbalimbali.

Rona-Look-alike-700x453

Kutoka kushoto Gokmen Akdogan na Cristiano Ronaldo

2- Wayne Rooney anafananishwa na Aaron Ashmore

Kama umepata bahati ya kuangalia Warehouse na Smallville kuna jamaa anaitwa Aaron Ashmore anafanishwa na Wayne Rooney wa Manchester United, ni mzaliwa Canada lakini ni maarufu nchini U.S.A

Rooney-look-alik

Kutoka kushoto ni Aaron Ashmore na Wayne Rooney

3- Ulishawahi kusikia headlines za Lionel Messi kuhusishwa kubadili dini? basi kuna jamaa anaitwa Abdul Karim kutokea Afghanistan alionekana kavaa jezi ya Lionel Messi na kuingia msikitini, hivyo wengi walianza kuhisi staa wa FC Barcelona Lionel Messi amebadili dini, anatajwa kwa kiasi kikubwa kufanana na Lionel Messi.

Messi-look-alike

Kutoka kushoto ni Abdul Karim na Lionel Messi

4- Demba Ba anafananishwa na Tyrese Gibson, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Demba Ba anatajwa kufanana na jamaa aliyecheza katika movie ya Fast and Furious Tyrese Gibson.

Ba-Gibson

Demba Ba na Tyrese Gibson

KINA NANI WAMEFANANA ZAIDI HAPA? NIACHIE COMMENT YAKO MTU WANGU

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments