Habari za Mastaa

Ali Kiba kayajibu matano, ishu ya beef, ubalozi wake, Tuzo sita, yeye na Diamond..

on

CFM II

Staa wa hits za ‘Cheketua na ‘Mwana’ ambazo zilimrudisha kwa nguvu kwenye muziki TZ, Ali Kiba alikuwa kwenye show ya XXL leo July 09 2015, kuna vitu vingi vinaendelea, leo kapata nafasi kuyajibu haya matano.

CFM

Ali Kiba na B12 kwenye XXL leo mchana.

Hivi ndio alivyoupata mchongo wa kuwa Balozi wa Kampeni ya WildAid >>> “Wanaangalia mtu ambaye anaeleweka, anayeweza kuwaambia watu wakaelewa jinsi ya kuzuia ujangili.. Lupita ni mfano, tayari amekuwa staa mkubwa sana watu wengi wanamuangalia

Ali Kiba

Ali Kiba akisalimiana na Lupita Nyong’o

Haya ndio majibu yake kuhusu sababu za kuamua kufanya daladala tour >>> “Nina imani kuna wanaonipenda na hawajawahi kuniona.. walipiga kura Tuzo za Watu, KTMA.. nilianzia Mnazi Mmoja mpaka Mtoni Mtongani, tukaenda Temeke, tukaja Ilala, Magomeni, Ubungo na Manzese mpaka Makumbusho

Maswali yalioulizwa zaidi na watu ndani ya daladala yalihusu nini? >>> “Iliulizwa kama nina beef na Diamond, pongezi za tuzo.. Watu walifurahishwa na tour yangu, hawakutegemea

Screen-Shot-2015-06-24-at-3.02.57-PM (1)

Ali Kiba kwenye Daladala Tour

Alitarajia kupata Tuzo zote sita KTMA 2015? >>> “Yeah… nilitarajia itakuwa hivyo, nafanya kazi nzuri na kutegemea watu watafurahia.. Naona nastahili Tuzo zote

Ni kweli hamsapoti Diamond kwenye MTV? >>> “Nilipotaka kutoa video yangu wasanii wengi niliwatumia picha walisapoti na wengine hawakunisapoti.. Mimi ni balozi ninayewakilisha Tanzania, ni kubwa sana na mimi nipo watu wanachukulia poa kwanini?“>>> Ali Kiba.

KIBA

Mimi sijalipiza kisasi, wengi wananitumia kazi zao nawasapoti.. Kwa ujumla Tanzania kuna tabia ya kutopeana support, lazima tukae pamoja watu wote angalau tuwe na semina tuwe Wazalendo… Mengi tumeyaona, Marehemu Kanumba alikosea kidogo kwenye BBA watu wakatafuta sehemu ndogo aliyokosea wakaandika”>>> Ali Kiba.

Sauti ya Ali Kiba iko haoa akijibu maswali yote kwenye XXL @CloudsFM

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments