Mmoja wa wahasiriwa wa Sean “Diddy” Combs, amefichua maelezo ya kutatanisha ya ubakaji katika filamu iliyopewa jina la Diddy: The Making of a Bad Boy.
Filamu hiyo imepangwa kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Januari 14.
Filamu ambayo inatarajiwa kuweka wazi baadhi ya madhambi ambayo msaani na mwanafilamu tajika P-diddy aliyafanya sasa inasubiriwa kwa hamu na ghamu ikitarajiwa kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kupitia Peacock.
Kionjo cha ‘’The Making of a Bad Boy’’ imefichua kuwa watu wa karibu wa Combs, akiwemo mlinzi wake wa zamani, mfanyakazi wa ndani, msanii wa kupodoa na mtayarishaji ni miongoni mwa wanaohojiwa kwenye filamu hiyo.
Mwimbaji na mtayarishaji wa nyimbo na filamu Al B, atazungumza kwa mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na Kim Porter kabla hajachumbiana na Combs
Itakumbukwa kuwa Combs pia amekabiliwa na mashtaka zaidi ya 25 ya madai yake ya utovu wa maadili ya ngono miongoni mwa madai mengine.
Msaani huyo mwenye umri wa miaka 55 anazuiliwa katika gereza la Metropolitan Detention Center huko Brooklyn, New York, tangu Septemba, alipokamatwa kwa makosa ya biashara ya ngono na ulaghai. Majaji watatu tofauti wamemnyima dhamana kwa nyakati tatu tofauti.
Mawakili wa Sean “Diddy” Combs hata hivyo walikosoa filamu hiyo katika taarifa waliotoa kupitia jarida la Newsweek siku ya Ijumaa.