Michezo

Aliyefanya jaribio la kuwapora Ozil na Kolasinac kahukumiwa miaka 10 jela

on

Moja kati ya matukio makubwa yaliojitokeza katika soka kwa mwaka 2019 ni pamoja na tukio la jaribio la uvamizi lililokuwa linawahusu wachezaji wa Arsenal Mesut Osil na rafiki yake Kolasinac.

Kijana Ashley Smith mwenye umri wa miaka 30 July 2019 akiwa na mwenzake Jordan Northover walifanya jaribio la kutaka kuwaibia kwa mabavu Ozil na Kolasinac.

Leo imetangazwa kuwa Ashley Smith kwa jaribio hilo amehukumiwa kwenda jela miaka 10 wakati mwenzake Jordan bado anasubiri hukumu, hata hivyo Ashley Smith ni mwizi mbobezi anahukumiwa miaka 10 jela wakati akiwa nje kwa uangalizi maalum baada ya kuwa na kifungo kingine cha miaka 3 na miezi sita (miezi 42) kwa kosa la wizi tena alilofanya 2017.

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments