Michezo

Aliyembagua Balotelli kafungiwa miaka mitano

on

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 38 amefungia kwa miaka mitano kutohudhuria shughuli yoyote ya kimichezo, baada ya kukutwa na hatia ya kumbagua mshambuliaji wa Brescia Mario Balotelli.

Katika tukio hilo lililotokea November 3 2019 limetolewa maamuzi jana, ikiwa Polisi wa Verona wamepitia na kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na ubaguzi huo uliofanya Balotelli akamate mpira ukiwa mchezoni na kuupiga nje.

Kitendo cha kuupiga nje mpira Balotelli na kutishia kususia mchezo kulifanya mchezo huo kusimama kwa dakika kadhaa kabla ya Balotelli kushawishiwa ma kuendelea na mchezo.

Soma na hizi

Tupia Comments