Michezo

Aliyempiga chupa Payet kwenda jela miezi 6

on

Kwa mujibu wa RMC Sports wameripoti kuwa waendesha mashitaka wa kesi ya shabiki Wilfred Serriere (32) wa Lyon ya kumpiga chupa mchezaji wa Marseille Dimitri Payet wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa wametaka shabiki huyo afungwe jela miezi sita pamoja na kutoingia uwanjani kwa miaka mitano.

Kutokana na tukio hilo lililotokea juzi mjini Lyon, uwanja wa Lyon sasa utafungwa kucheza mechi ukiwa na mashabiki hadi uchunguzi ukamilike.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri tukio la Payet kupigwa chupa na shabiki wa Lyon lilitokea Jumapili ya November 21 dakika ya 5 wakati wa mchezo wa Lyon vs Marseille, wakati Payet anaenda kupiga kona ndio shabiki akampiga na chupa.

Soma na hizi

Tupia Comments