Mahakama ya Mwanzo wilaya ya Kwimba Ngudu mjini imemuhukumu Erasto Bonda (33) kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa moja lenye mashtaka mawili, kutoa lugha ya matusi pamoja na kuzusha taarifa za uongo dhidi ya Nyakia Chirukile Katibu Tawala wilaya ya Kwimba.
Kesi hiyo ya jinai namba 16, 2023 iliyofunguliwa na ndugu Nyakia Chirukile ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya (DAS) katika Mahakama ya Mwanzo wilaya ya Kwimba.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mwanzo Ngudu Kwimba Michael Turuka, Leo march 27, 2023 ametoa hukumu hiyo mara baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili na kumtia hatiani Mshtakiwa Erasto Bonda kwa Mashtaka yote mawili na kumuhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kila shtaka na adhabu zote zinataenda pamoja na kuthibitishwa na Mahakama ya wilaya kwa kuwa Mshtakiwa amefungwa zaidi ya miezi sita.
Mshtakiwa Erasto Boda inaelezwa kwa nyakati tofauti alimtusi na kumzushia uwongo Katibu Tawala Kwimba Nyakia Chirukile kwenye mitandao ya kijamii (ma group ya WhatsApp) kuwa ameiba fedha za Serikali zaidi ya mil. 200, pamoja na kuleta Waganga wa jadi kutoka Tanga na Kigoma kwenye nyumba za Serikali kumuosha dawa.