Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limethibitisha kumwachia kwa dhamana John Isaya (21), mkazi wa Bukala wilaya Sengerema, anayekabiliwa kwa tuhuma za kutangaza kuuza mtoto wake kwa shilingi milioni moja na laki sita ( 1,600,000/-), mitandaoni.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP. Wilbrod Mutafungwa, wakati akizungumza na @Ayo_TV mtuhumiwa ameruhusiwa kuwa nje kwa dhamana kutokana na aina ya tuhuma zinazomkabili kuruhusu dhamana kisheria.
Mutafungwa ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kwa kina kuhusu tukio hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, huku akisisitiza kuwa pindi uchunguzi utakapokamilika, hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
January 04, Jeshi la Polisi huko wilaya ya Sengerema lilifanikiwa kumkamata John Isaya Dereva Bajaji akituhumiwa kutumia mitandao ya kijamii TikTok, kusambaza taarifa za madai ya kuuza mtoto wake kwa lengo la kutafuta umaarufu.