Mwanamume wa Missouri ambaye alivamia na lori la kukodi kwenye lango karibu na Ikulu ya White House akiwa na matarajio ya kupindua serikali ahukumiwa kifungo cha miaka nane gerezani siku ya Alhamisi, waendesha mashtaka walisema.
Sai Varshith Kandula, 20, wa St. Louis, alikiri hatia mnamo Mei kwa shtaka moja la kuiba kimakusudi au kupora mali ya Marekani katika tukio la Mei 22, 2023.
Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani kwa Washington ilisema lengo lake lilikuwa “kupindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Marekani ili kuchukua nafasi yake na udikteta unaochochewa na itikadi ya Nazi.”
Kandula, raia wa India ambaye alikuwa mkazi halali wa kudumu wa Marekani aliyekuwa na kadi ya kijani wakati huoalifanya tukio hilo kimakusudi hii ni kulingana na mahakama.