Mwanamke wa Alabama ambaye anadai alibakwa na Jay-Z na Sean Diddy Combs alipokuwa na umri wa miaka 13 anaweza kuendelea na kesi yake bila kujulikana utambulishi wake, angalau kwa sasa.
Jaji wa Manhattan aliamua Alhamisi kwamba mwanamke huyo anaweza kubaki bila kutambuliwa katika hatua za mwanzo za kesi hiyo lakini anaweza kuhitajika kufichua utambulisho wake baadaye ikiwa kesi hiyo itasonga mbele.
Uamuzi huo ulikuja na karipio kali kwa wakili wa Jay-Z, ambaye alikosolewa kwa kutumia lugha ya ugomvi katika kesi mahakamani.
Wakati huo huo, Diddy bado yuko jela huko New York, akikabiliwa na mashtaka ya biashara ya ngono na wimbi la kesi za unyanyasaji wa kijinsia. Kesi hizi, zilizowasilishwa na wakili Tony Buzbee, zinadai unyanyasaji katika karamu huko New York, California, na Florida, mara nyingi huhusisha vinywaji vyenye dawa za kulevya.