Almasi kubwa ya karati 2,492 ya pili kwa ukubwa duniani imegunduliwa nchini Botswana, kampuni ya uchimbaji madini ya Kanada iliyopata jiwe hilo ilitangaza Alhamisi.
Almasi hiyo iligunduliwa katika mgodi wa almasi wa Karowe kaskazini mashariki mwa Botswana kwa kutumia teknolojia ya kugundua kupitia X-ray, Lucara alisema katika taarifa yake.
Lucara hakutoa makadirio ya thamani ya almasi hiyo .
Kwa upande wa jiwe hilo ni la pili baada ya almasi ya Cullinan yenye karati 3,106 iliyogunduliwa nchini Afrika Kusini mnamo 1905.
“Tuna furaha kubwa kuhusu kupatikana kwa almasi hii ya ajabu ya karati 2,492,” rais wa Lucara William Lamb alisema katika taarifa hiyo.
Ugunduzi huu ulikuwa “mojawapo ya almasi kubwa zaidi kuwahi kuibuliwa” na kugunduliwa kwa kutumia teknolojia ya X-ray ya kampuni ya Mega Diamond Recovery iliyowekwa mnamo 2017 kutambua na kuhifadhi almasi kubwa za thamani ya juu, ilisema taarifa hiyo.